Write For Us

Filimbi ya Kasa: Learn Swahili with subtitles - Story for Children and Adults "BookBox.com"

E-Commerce Solutions SEO Solutions Marketing Solutions
140 Views
Published
Turtle, a gifted flutist, is trapped by a greedy man. How will she escape now?

Filimbi ya Kasa
Hadithi ya ki Brazili
Na inasimuliwa na BookBox
Hapo zamani za kale,
kulikuwa na Kasa aliyepiga
filimbi kwenye kingo ya mto.
Wakati Kasa alipokuwa akipiga
filimbi,
wanyama kama simba, ndovu,
vipepeo, nyoka na hata tumbili
walicheza mziki wake.
Siku moja, mwanamume mmoja
alisikia mziki wa Kasa,
“Aah!,” aliwaza,
“Huyo anawezekana kuwa
ni Kasa anapiga mziki,
Kasa anaweza kuwa mtamu sana
wakati huu.”
Kwa hivyo, akamwita:
“Kasa! Hebu nionyeshe
filimbi yako nzuri.”
Basi Kasa alitembea pole pole
hadi mlangoni na
kunyosha filimbi yake.
Lakini mara tu
yule mwanamume alipomwona Kasa,
alimshika shingo
na kuanza kukimbia.
Kasa alianza kulia
ili apate usaidizi,
lakini hakuweza kutoa sauti.
Kwa hivyo alifunga macho yake
na kushikilia filimbi yake,
kwa nguvu na kutarajia bahati nzuri.
Mwanamume yule alipofika
nyumbani mwake
alimueka Kasa ndani
ya kibanda na kumfungia.
Kisha akawageukia wanawe
na kuwaambia, “Msimuwachilie Kasa
atoke nje ya kibanda.”
Halafu akaenda zake shambani.
Watoto walianza kucheza
nje ya nyumba,
ilhali wakati huo
Kasa alikuwa amenyamaza
ndani ya kibanda alimofungiwa,
huku akifikiria maneno
aliyosema yule mwanamume
kwa watoto wake.
Basi akaanza kupiga wimbo mzuuuri
kwa kutumia filimbi yake,
na mara tu
watoto waliposikia ule mziki wa Kasa,
walikimbilia kibanda
alimowekwa Kasa
na kumuliza, “Kasa?
ni wewe unayepiga filimbi?”
huku macho yao
yakiwa wazi kwa mshangao.
“Ndio ni mimi” Kasa alisema.
Huku akiendelea kupiga filimbi,
kwa kuwa alikuwa amewaona watoto,
nao wamefurahi kusikia.
Na badaaye aliacha kupiga
na kuwambia wale watoto
“Mnajua naweza cheza vizuri zaidi
kuliko kupiga filimbi?
je mungependa kuona?”
“Oh tafadhali!” yule kijana mdogo
alisema kwa machozi ya furaha.
“Basi nitawaonyesha jinsi ya kucheza
na kupiga filimbi kwa wakati mmoja,”
Kasa alisema,
“Lakini, kabla niwaonyeshe
lazima munifungulie
nitoke ndani ya hichi kibanda.
Kwani hamna nafasi nzuri.”
Basi, yule kijana mdogo
akafungua kile kibanda
alimokuwa amefungiwa Kasa
na Kasa akaanza kucheza
huku akipiga filimbi.
Watoto walicheka
na kupiga makofi,
kwani hawa kuwa wamewahi kuona
jambo la kufurahisha kama lile.
Baadaye Kasa aliacha kucheza.
Huku wale watoto wakimwambia,
“Usiache kucheza!”
“Aah!” Kasa alilalamika,
“miguu yangu imekakamaa,
na kama mta niruhusu
nitembee kidogo
ili miguu yangu itangamae.”
“Lakini usiende mbali,”
yule mtoto wa kike alimwonya Kasa,
“tena urudi sasa hivi.”
Kasa akasema “Msijali,
ninyi ningojeni hapa.”
Kisha Kasa akatambaa
na kuelekea msituni.
Punde tu alipokuwa
hayupo tena machoni,
Kasa alikimbia kwa kasi
hadi nyumbani kwake.
Na tangu siku hiyo
hakuna aliyemwona Kasa tena.
Na hadi leo hii,
ukitega masikio yako vizuri
utaweza kusikia sauti nzuri
ya filimbi ikilia kutoka msituni.

Author: Amit Garg
Illustrations: Emanuele Scanziani
Music: Holger Jetter
Translator & Narrator: Sharon Mbeyu
Animation: BookBox

FREE Apps for iPads & iPhones: http://www.bookbox.com/ios
FREE Apps for Android phones & tablets: http://www.bookbox.com/android
Many more stories, languages & multiple subtitle options: http://www.bookbox.com

#BookBox #BookBoxSwahili #Learn2Read
Category
English Languages
Sign in or sign up to post comments.
Be the first to comment